43

No.14

Sheria ya Makosa ya Mtandao

2015

mfumo wa optika au katika aina nyingine ya mfumo
inayofanana na hiyo;
“ kifaa cha TEHAMA katika uchunguzi ” maana yake ni
kifaa cha uchunguzi au kifaa kinachojumuisha mianzi
laini au mianzi ngumu iliyowekwa kwenye au
inayohusiana na mfumo wa kompyuta au sehemu ya
mfumo wa kompyuta na inayotumika kutekeleza kazi
zinazojumuisha uingiaji kwa siri au ukusanyaji wa
taarifa za kiuchunguzi zinazohusiana na matumizi ya
kompyuta au mfumo wa kompyuta;
“zuia” kuhusiana na mfumo wa kompyuta inajumuisha(a) kusababisha kuingiliwa kielektromagnetiki kwa
mfumo wa kompyuta;
(b) kuvuruga mfumo wa kompyuta, kwa namna
yoyote ile; au
(c) kuingiza, kutuma, kuzorotesha, kufuta, kuvuruga,
kubadilisha au kuzuia data kompyuta;
“mtunza data” maana yake ni mtu anayetoa huduma ya
kusambaza data kwa kutunza taarifa inayotolewa na
mtumiaji wa huduma hiyo;
“kiunganishi tovuti” maana yake ni alama, neno, kirai,
sentensi au taswira iliyo katika tovuti au taarifa
inayokuhusiana na chanzo kingine kinachosababisha
kuounyesha au kufunguka kwa tovuti nyingine;
“haki bunifu’’
maana yake ni haki zinazotokana au
zinazohusiana na haki miliki, hati bunifu, alama za
biashara na mambo mengine yanayohusiana nayo;
“kuingilia” kuhusiana na utendaji kazi wa kompyuta
inajumuisha upatikanaji, utazamaji, usikilizaji au
kunukuu data kompyuta yoyote ya mawasiliano ya
kompyuta au mifumo ya kompyuta kwa njia yoyote
ya kielektroniki;

Select target paragraph3