Na.14
Sheria ya Makosa ya Mtandao
2015
40
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
NA.14 YA 2015
NAKUBALI,
JAKAYA MRISHO KIKWETE
Rais
25 Aprili, 2015
Sheria inayoainisha masharti yanayohusu makosa yanayohusiana na
matumizi ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano; kuainisha utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na
matumizi ya ushahidi wa kielektroniki na masuala mengine
yanayohusiana na hayo.
[………….]
IMETUNGWA na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
SEHEMU YA KWANZA
MASHARTI YA UTANGULIZI
Jina na tarehe
ya kuanza
kutumika
1. Sheria hii itaitwa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya
mwaka 2015, na itaanza kutumika tarehe ambayo Waziri,
kwa Tanzago la Serikali katika Gazeti la Serikali.
Matumizi
2. Isipokuwa kwa kifungu cha 50, Sheria hii
itatumika Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.