47
No.14
Sheria ya Makosa ya Mtandao
2015
(2) Mtu ambaye(a) anawasilisha, anafichua au anasambaza data
kompyuta, programu ya kompyuta, ishara ya
kuingilia
au
anaagiza
mtu
ambaye
hajaidhinishwa;
(b) kwa makusudi na kinyume cha sheria anapokea
data kompyuta ambayo haijaidhinishwa,
ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika, kulipa faini
isiyopungua shilingi milioni mbili au mara tatu ya thamani
ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria au yoyote
iliyokubwa, au kutumikia kifungo kwa kipindi
kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.
(3) Mtu ambaye kwa makusudi na isivyo halali
ataharibu au atabadili data yoyote ya kompyuta, iwapo data
hiyo inatakiwa kutunzwa kisheria au ni ushahidi kwenye
shauri lolote chini ya Sheria hii kwa(a) kuharibu au kubadilisha data, programu au aina
nyingne yoyote ya taarifa iliyoko ndani au nje ya
mfumo wa kompyuta;
(b) anawasha, anaingiza au anapakua programu
ambayo imetengenezwa kwa lengo la kuharibu,
au kubadilisha data, programu au aina nyingine
yoyote ya taarifa iliyoko ndani au nje ya mfumo
wa kompyuta; au
(c) anatengeneza, anabadilisha au anaharibu namba
ya siri, namba binafsi ya utambulisho au namna
inayotumika kuingika kwenye mfumo wa
kompyuta,
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika
kulipa faini isiyopungua shilingi milioni ishirini au mara
tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria,
au yoyote iliyokubwa, au