Na.14
Sheria ya Makosa ya Mtandao
kutumikia kifungo kwa kipindi
mmoja au vyote kwa pamoja.
2015
48
kisichopungua mwaka
Ujasusi data
Sura ya 47
8.-(1) Bila kuathiri masharti ya Sheria ya Usalama
wa Taifa, mtu hataingilia na kujipatia data kompyuta
iliyokingwa dhidi ya uingiaji bila idhini.
(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1)
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika
kulipa faini isiyopungua shilingi milioni ishirini au mara
tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria au
yoyote iliyokubwa, au kutumikia kifungo kwa kipindi
kisichopungua miaka mitano au vyote kwa pamoja.
Kuingilia
mfumo
kinyume cha
sheria
9. Mtu ambaye, kwa makusudi na kinyume cha
sheria anazuia au anaingilia(a) utendaji kazi wa mfumo wa kompyuta;
(b) matumizi au uendeshaji wa mfumo wa
kompyuta,
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika
kulipa faini isiyopungua shilingi milioni mbili au mara tatu
ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au
yoyote iliyokubwa au kutumikia kifungo kwa kipindi
kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.
Kifaa kisicho
halali
10.-(1) Mtu hatajishughulisha na, au kumiliki,
kinyume cha sheria(a) kifaa, ikijumuisha programu ya kompyuta
iliyotengenezwa
au
inayotumiwa
kwa
madhumuni ya kutenda kosa;
(b) namba ya siri ya kompyuta, ishara ya kuingilia
au data inayofanana na hiyo ambayo inaweza
kutumika na