Na.14

Sheria ya Makosa ya Mtandao

2015

46

(ii)

mawasiliano yasiyo ya umma ya
kieletromaniginetiki
yatokanayo
katika mfumo wa kompyuta usio wa
umma; au
(iii)
mfumo wa kompyuta usio wa umma
ambao umeunganishwa na mfumo
mwingine wa kompyuta; au
(b) anakwepa hatua za udhibiti zilizoelekezwa kwa
ajili ya kukinga kuingiliwa kwa maudhui
yaliyomo kwenye mawasiliano yasiyo ya umma.
(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1)
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika
kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tano au kutumikia
kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote
kwa pamoja.
Kuingilia data
kinyume cha
sheria

7.-(1) Mtu ambaye kwa makusudi na kinyume cha
sheria(a)
(b)
(c)
(d)

anaharibu au anazorotesha data kompyuta;
anafuta data kompyuta;
anabadili data kompyuta;
anaifanya data kompyuta ipoteze maana,
ishindwe kutumika au ikose ufanisi;
(e) anazuia au anaingilia matumizi halali ya data
kompyuta;
(f) anamzuia au anamuingilia mtu mwingine
anayetumia data kompyuta kihalali; au
(g) anamzuia mtu aliyeidhinishwa kutumia data
kompyuta,
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika
kulipa faini isiyopungua shilingi milioni kumi au mara tatu
ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume na sheria au
kutumikia, au yoyote iliyokubwa kifungo kwa kipindi
kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja.

Select target paragraph3