45
No.14
Sheria ya Makosa ya Mtandao
2015
SEHEMU YA PILI
MASHARTI YANAYOHUSIANA NA MAKOSA NA ADHABU
Kuingia
kinyume cha
sheria
4.-(1) Mtu hataingia au kusababisha kuingiliwa
mfumo wa kompyuta kinyume cha sheria na kwa makusudi.
(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1)
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika
kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au mara tatu ya
thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria au
yoyote iliyokubwa, au kutumikia kifungo kwa kipindi
kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.
Matumizi ya
mfumo wa
kompyuta
kinyume cha
sheria
5.-(1) Mtu hatatumia au kuendelea kutumia mfumo
wa kompyuta, kinyume cha sheria na kwa makusudi, baada
ya kuisha kwa muda ambao aliruhusiwa kutumia mfumo wa
kompyuta.
(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1)
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika
kulipa faini isiyopungua shilingi milioni moja au mara tatu
ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria au
yoyote iliyokubwa, au kutumikia kifungo kwa kipindi
kisichopungua miezi sita au vyote.
Kuingilia
mawasiliano
kinyume cha
sheria
6.-(1) Mtu ambaye, kwa makusudi na kinyume cha
sheria(a) anaingilia kwa kutumia njia ya kiufundi au kwa
njia nyingine yoyote:
(i)
mawasiliano yasiyo ya umma kwenda
au kutoka au yaliyo ndani ya mfumo
wa kompyuta;