Na.14

Sheria ya Makosa ya Mtandao

2015

44

“afisa utekelezaji wa sheria” maana yake ni afisa wa polisi
mwenye cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa polisi,au
cheo cha juu ya hicho au mpelelezi, afisa Usalama
wa Taifa mwendesha mashtaka, au afisa muidhiniwa
wa mamlaka yenye dhamana na mawasiliano au mtu
mwingine yeyote aliyeidhinishwa chini ya sheria
yoyote;
“Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana na
masuala
ya Habari na Teknolojia ya Habari.
“kuchapisha” maana yake ni usambazaji, uwasilishaji,
uwekaji wazi, ubadilishanaji,uchapishaji, uonyeshaji, nakili,
uuzaji au utoaji kwa ajili ya mauzo, kukodisha au usambazaji
wa aina yoyote ile;
“mali” maana yake ni mali ya aina yoyote inayotembelea au
la, inayogusika au isiyogusika na inajumusha:
(a) fedha yoyote inayotumika au isiyotumika katika
Jamhuri ya Muungano Tanzania;
(b) taarifa, ikijumuisha programu unayotolewa
kielektroniki, data au nakala zake, zinazoweza
kusomwa na binadamu au kwa kompyuta; au
(c) haki yoyote au maslahi kwenye mali;
“ubaguzi” maana yake ni taarifa za namna yoyote zinazokuza
au kuchochea chuki, ubaguzi au vurugu dhidi ya mtu
yeyote au kundi la watu kwa msingi wa tabaka, rangi,
asili,utaifa, kabila au dini;
“mtoa huduma” maana yeke ni mtu au upande unaowezesha
mfumo wa taarifa kupatikana kwa mtu wa tatu.

Select target paragraph3