69
No.14
Sheria ya Makosa ya Mtandao
2015
au mfumo mwingine wa usimamizi uliotajwa
chini ya sheria yoyote;
(c) uliyotolewa na sheria au amri ya mahakama ili
kutoa, kuzuia au kukataza uingiaji kwenye
mawasiliano ya kieletroniki au kusitisha au
kuzuia kitendo kisicho cha halali.
SEHEMU YA SITA
MASHARTI YA JUMLA
Kinga
47.-(1) Bila ya kujali sheria nyingine yoyote
kinyume na haya, jambo au kitu chochote kitakachofanywa
na afisa utekelezaji wa sheria, katika utekelezaji wa
majukumu yake chini ya Sheria hii, hakitasababisha afisa
utekelezaji wa sheria kuwajibika binafsi kwa jambo au kitu
hicho.
(2) Mtu hatawajibika kuhusiana na utekelezaji wa
kitendo chochote au kutokutenda, iwapo kitendo hicho au
kutokutenda huko kulifanywa kwa nia njema na si kwa
uzembe kwa mujibu wa masharti ya Sheria hii.
Utaifishaji
mali
48.-(1) Pamoja na adhabu iliyotolewa chini ya
Sheria hii, mahakama inaweza kutoa amri kwa ajili ya
utaifishaji wa(a) mali yoyote inayoonekana kuwa ni sehemu ya
mapato yatokanayo na kosa; na
(b) chombo au mali yoyote iliyotumika au
inayokusudiwa kutumika kutenda au kufanikisha
utendaji wa kosa.
(2) Pamoja na amri iliyotolewa chini ya kifungu
kidogo cha (1), mahakama inaweza kumuamuru mtu
aliyetiwa hatiani kumlipa fidia mtu aliyeathirika na kosa
hilo kwa kadri ambavyo mahakama itaona inafaa.