Na.14
Sheria ya Makosa ya Mtandao
2015
70
Makosa
yanayofanywa
na kampuni
hodhi
49. Endapo kampuni inatiwa hatiani kwa kosa chini
ya Sheria hii, mtu yeyote ambaye wakati wa utendaji wa
kosa(a) alikuwa ni mkurugenzi, afisa au vinginevyo
anahusika na mambo ya utawala wa kampuni
hodhi hiyo;
(b) huku akiwa anajua, aliruhusu kitendo
kilichopelekea kosa hilo atachukuliwa kuwa
ametenda
kosa
hilo,
isipokuwa
kama
itathibitishwa wakati kosa hilo linatendeka,
lilitendeka bila idhini yake na alifanya jitihada za
kutosha kuzuia kutendeka kwa kosa hilo,
atachukuliwa kuwa ametenda kosa hilo na
anaweza kushitakiwa na kuadhibiwa ipasavyo.
Kufifilisha
kosa
50.-(1)
Bila ya kuathiri sheria nyingine
inayotumika Tanzania Bara, Mkurugenzi wa Mashtaka,
anaweza, muda wowote kabla ya mwenendo wa mahakama
kuanza na kwa kuzingatia tamko la kukiri kosa kwa hiari la
mshitakiwa anaweza kufifilisha kosa na kuamuru mtu huyo
alipe kiasi cha pesa atakachokitaja ambacho hakitazidi kiasi
cha faini kwa kosa lolote hilo.
(2) Amri ya kufifilisha kosa chini ya kifungu kidogo
cha (1) itakuwa (a) ki maandishi, ikiainisha kosa lililotendeka, kiasi
cha fedha zitakazolipwa na tarehe ya kufanya
malipo ikiambatanisha tamko la kukubali kosa
lililorejewa chini ya kifungu kidogo cha (1);
(b) ni uamuzi wa mwisho na hautakatiwa rufaa; na
(c) na uwezo wa kutekelezwa katika namna sawa na
amri ya Mahakama Kuu.