Na.14

Sheria ya Makosa ya Mtandao

2015

68

(a)
(b)
(c)
(d)

majina kamili na anuani;
saini ya mlalamikaji;
maelezo ya haki inayodaiwa kuvunjwa;
maelezo juu ya kitu au shughuli ambayo
inadaiwa kuwa chimbuko la kitendo kilicho
kinyume na sheria;
(e) hatua ya utatuzi inayotakiwa kuchukuliwa na
mtoa huduma kuhusiana na lalamiko;
(f) maelezo kuwa mlalamikaji anafanya hivyo kwa
nia njema;
(g) maelezo ya mlalamikaji kuwa, kwa ufahamu
wake,
taarifa
iliyomo
kwenye
taarifa
zilizochukuliwa ni sahihi.
(3) Mtu anayewasilisha taarifa kwa mtoa huduma
kuhusiana na muamala usio halali, huku akijua kuwa taarifa
hiyo ni potofu, atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani,
atatakiwa kulipa faini ya shilingi million tano au kifungo
cha mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.
(4) Mtoa huduma atakayeshindwa kuchukua hatua
juu ya notisi ya kuondoa aliyoipokea kwa mujibu wa Sheria
hii, atashitakiwa kwa kosa la kuainisha taarifa chini kifungu
kidog cha (1).
(5) Mtu anayetoa notisi ya kuondoa kwa mtoa
huduma, na mtoa huduma akashindwa kufanyia kazi notisi
hiyo, mtu huyo anaweza kutoa taarifa kwa mamlaka husika
kwa kushindwa kutekeleza notisi na mamlaka husika
inaweza kumchukulia hatua mtoa huduma au kumtaka mtoa
huduma huyo kuifanyia kazi notisi hiyo au kuchukua hatua
yoyote kulishughulikia suala hilo.
(6) Mtoa huduma hatawajibika kwa kuondoa taarifa
ikiwa ameifanya kwa mujibu wa Sheria hii.
Wajibu
mwingine
kutoadhiriwa
na sheria

46. Sehemu hii haitaathiri wajibu wa mtoa huduma:
(a) uliyotolewa kwa makubaliano;
(b) ambaye anatenda kwa namna hiyo chini ya leseni

Select target paragraph3