67

No.14

Sheria ya Makosa ya Mtandao

2015

(b) baada ya kufahamu kuwa taarifa zilizo kinyume
na sheria zilizotunzwa kwa njia nyingine zaidi ya
amri ya mamlaka ya umma, haraka
iwezekanavyo anaitaarifu mamlaka husika.
Mtoa huduma
ya utafutaji wa
taarifa

44.-(1) Mtoa huduma ya utafutaji wa taarifa
hatawajibika kwa matokeo ya utafutaji huo, kwa masharti
kwamba(a) haanzishi mawasiliano;
(b) hachagui mpokeaji wa mwasiliano; na
(c) hachagui au kubadilisha taarifa iliyoko kwenye
mawasiliano.
(2) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, “mtoa
huduma ya utafutaji wa taarifa” maana yake ni mtu
anayetengeneza au anayeendesha huduma ambayo inatafuta
taarifa inayotengeneza kiashiria cha taarifa za mtandao au
anawezesha upatikanaji wa vifaa vya kielektroniki kwa ajili
ya utafutaji wa taarifa inayotolewa na mtu wa tatu.

Notisi ya
kuondoa

45.-(1) Mtu anaweza, kupitia notisi ya kuondoa,
kumtaarifu mtoa huduma kuhusu(a) data au taarifa iliyomnyima mpokeaji au mtu wa
tatu haki ya huduma;
(b) vitu au shughuli yoyote ambayo ni kinyume cha
sheria; au
(c) suala lolote linalotekelezwa au linalotolewa
kinyume cha Sheria hii au sheria nyingine.
(2) Kwa madhumuni ya Sehemu hii, notisi ya
kuondoa itakuwa katika hali ya kudumu ikitumwa na
mlalamikaji kwenda kwa mtoa huduma au wakala wake, na
itajumuisha-

Select target paragraph3