Na.14
Sheria ya Makosa ya Mtandao
2015
66
ambapo mpokeaji anafanya hivyo chini ya mamlaka
ya mtoa huduma.
Mhifadhi data
kwa muda
mfupi
42. Mtoa huduma ya kuhifadhi data hatawajibika
kwa ajili ya utunzaji wa taarifa ikiwa(a) habadilishi taarifa;
(b) anatekeleza masharti ya utoaji wa uwezo wa
kuingia kwenye mfumo;
(c) anazingatia kanuni zinazohusu na uboreshaji wa
taarifa;
(d) haiingiliani na matumizi halali ya teknolojia
inayotambulika na wengi na inayotumika sokoni
kupata data kwa ajili ya matumizi ya taarifa
hiyo; na
(e) anachukua hatua za haraka kuondoa au kusitisha
matumizi ya au kufikiwa kwa taarifa ambayo
imetunzwa baada ya kupokea taarifa kamili
kwamba taarifa iliyo kwenye chanzo cha
mawasiliano imeondolewa kutoka kwenye
mtandao, au ufikiwaji wake umesitishwa au
matumizi yake yamesitishwa, au kwamba
mahakama au mamlaka husika imeamuru itolewe
au isitishwe.
Mtoa huduma
ya
kuunganisha
tovuti
43. Mtoa huduma ya kuunganisha tovuti
hatawajibika kwa taarifa aliyounganisha iwapo(a) haraka iwezekanavyo anaondoa au anasitisha
matumizi ya taarifa baada ya kupokea amri
kutoka kwa mamlaka husika ya kuondoa
kiunganishi hicho; na