65

No.14

Sheria ya Makosa ya Mtandao

2015

kompyuta au kuendesha vifaa kupitia mfumo wa kompyuta
ulio chini ya mamlaka yake kwa masharti kwamba mtoa
huduma(a) haanzishi urushaji mawasiliano;
(b) hachagui mpokeaji wa mawasiliano; au
(c) hachagui au habadilishi data iliyoko kwenye
mawasiliano.
(2) Mawasiliano na utoaji wa uwezo wa kuingia
kwenye mfumo wa kompyuta yaliyotolewa chini ya kifungu
kidogo cha (1) utajumuisha, utunzaji wa taarifa
iliyosambazwa
kwa
madhumuni
ya
kuendeleza
mawasiliano kwenye mfumo wa kompyuta kwa njia
inayojiendesha yenyewe kwa kupitia mtu kati na kwa muda
kwa kuzingatia kwamba mawasiliano yanafanyika kwa(a) madhumuni ya kuendesha na kusambaza taarifa
katika mfumo wa kompyuta;
(b) namna ambayo kwa kawaida haiwezi kupatikana
isipokuwa tu kwa mpokeaji mlengwa;na
(c) muda ambao sio mrefu sana zaidi ya muda
unaofaa kuwasilisha ujumbe husika kwa
mlengwa.
Mtunza Data

41.-(1) Mtunza data hatawajibika na taarifa
zilizohifadhiwa kwa maombi ya mtumiaji wa huduma hiyo,
kwa masharti kwamba(a) anaondoa au kusitisha mara moja upatikanaji wa
taarifa baada ya kupokea amri kutoka taasisi
yenye mamlaka au mahakama ya kuondoa taarifa
zilizo kinyume cha sheria; au
(b) baada ya kufahamu kuwa taarifa iliyohifadhiwa
iko kinyume cha sheria ataitaarifu mara moja
taasisi husika.
(2) Kifungu kidogo cha (1) hakitatumika pale

Select target paragraph3