Na.14
Sheria ya Makosa ya Mtandao
2015
64
mtoa huduma anaisambaza au kuhifadhi;
(b) hatafuta maelezo au mazingira yanayoonyesha
shughuli zinazofanywa kinyume na sheria.
(2) Waziri anaweza kuweka masharti yanayohusu
utaratibu wa watoa huduma kwa ajili ya(a) kutoa taarifa kwa mamlaka husika ya umma
kuhusiana na shughuli zilizo kinyume na sheria
zilizofanywa au taarifa inayotolewa na watumiaji
wa huduma zao; na
(b) kuzipatia mamlaka husika, kwa kuomba, taarifa
zitakazowezesha kuwatambua watumia huduma.
(3) Mtoa huduma hatawajibika kwa uwekaji wazi wa
data iliyotolewa kihalali kwa mtu wa tatu baada ya
kuthibitisha kwamba:
(a) mtu huyo wa tatu alitenda hivyo pasipo mtoa
huduma ya mtandao kufahamu; au
(b) mtoa huduma alitekeleza wajibu unaostahili na
alitumia ujuzi ili kuzuia uwekwaji wazi wa data
hizo.
(4) Endapo mtoa huduma atakuwa na uelewa juu ya
taarifa au kitendo cha kihalifu kwenye mfumo wa kompyuta
ambao upo chini ya udhibiti wake, atatakiwa(a) kuondoa taarifa kwenye mfumo wa kompyuta
uliyo chini ya udhibiti wa mtoa huduma;
(b) kusimamisha au kusitisha huduma inayohusu
taarifa au kitendo hicho;
(c) kutaarifu mamlaka husika juu ya kitendo au
taarifa hiyo, maelezo husika na utambuzi wa
mhusika anayepewa huduma.
Mtoa huduma
ya kuingia
kwenye mfumo
40.-(1) Mtoa huduma ya uwezo wa kuingia kwenye
mfumo hatawajibika kwa kurusha au kuendesha mfumo wa
kompyuta kwa ajili ya mtu wa tatu katika njia ya
mawasiliano yakielektroniki ambayo yeye ni mtoa huduma
tu ya kuwezesha kuingia kwenye mfumo wa