63
No.14
Sheria ya Makosa ya Mtandao
2015
uchunguzi;
(c) taarifa yoyote iliyopatikana;
(5)
Taarifa iliyopatikana chini ya kifungu hiki
italindwa dhidi ya mabadiliko, kufutwa bila ya idhini na
kuingia kwenye mfumo bila idhini.
(6) Idhini iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha
(1) itakuwa halali kwa kipindi cha siku kumi na nne.
(7) Mahakama inaweza, kwa maombi, kuongeza
muda uliotolewa chini ya kifungu kidogo cha (6) kwa
kipindi kingine cha siku kumi na nne au kwa kipindi kingine
kwa kadri itakavyoona inafaa.
(8) Iwapo mchakato wa uwekaji wa kifaa unahitaji
kutembelea eneo, masharti ya kifungu cha 30 yatatumika.
(9) Pamoja na amri iliyotolewa chini ya kifungu
kidogo cha (1), mahakama inaweza, kwa maombi,
kumuamuru mtoa huduma kuwezesha mchakato wa kuweka
kifaa cha kipelelezi.
(10) Waziri anaweza, kwa taarifa itakayochapishwa
kwenye Gazeti la Serikali, kuainisha makosa ambayo
mahakama inaweza kutoa amri ya kutumia kifaa cha
TEHAMA katika uchunguzi.
Usikilizaji wa
maombi
38. Utaratibu wa kusikiliza maombi kwa mujibu wa
Sehemu hii utafanywa kwa upande mmoja na kwa siri.
SEHEMU YA TANO
WAJIBU WA WATOA HUDUMA
Wajibu wa
ufuatiliaji
39.-(1) Wakati wa kutoa huduma chini ya Sehemu
hii, mtoa huduma(a) hatawajibika kufuatilia data ambayo