Na.14
Amri ya
mahakama

Matumizi ya
kifaa cha
TEHAMA
katika
uchunguzi

Sheria ya Makosa ya Mtandao

2015

62

36. Endapo ambapo utoaji data au utunzaji data wa
dharura chini ya vifungu vya 31, 32, 33, 34 au 35 kwa kadri
itakavyokuwa, hauwezi kufanyika bila kutumia nguvu au
kutokana na pingamizi kutoka kwa mtu mwenye kumiliki
data au thamani ya ushahidi katika data inaweza
kuhifadhiwa kwa amri ya mahakama, afisa utekelezaji wa
sheria anaweza kuomba mahakamani amri ya utoaji au
utunzaji wa data.
37.-(1)
Endapo afisa utekelezaji wa sheria
anaridhika kuwa ushahidi wa msingi hauwezi kukusanywa
kwa kutumia utaratibu ulioainishwa chini ya Sehemu hii,
afisa utekelezaji huyo anaweza kuiomba mahakama kutoa
amri ya kuidhinisha matumizi ya kifaa cha uchunguzi.
(2) Maombi yaliyotolewa chini ya kifungu kidogo
cha (1) yatajumuisha(a) jina na anwani ya mtuhumiwa;
(b) maelezo ya mfumo wa kompyuta unaolengwa;
na
(c) maelezo ya hatua zinazokusudiwa kuchukuliwa,
madhumuni, kiasi na muda wa matumizi
unaokusudiwa.
(3) Afisa utekelezaji wa sheria atahakikisha kuwa
mabadiliko yaliyofanywa kwenye mfumo wa kompyuta au
data iliyomo kwenye kompyuta ya mtuhumiwa zinajikita
kwenye marekebisho yaliyo ya msingi kwa ajili ya
uchunguzi
na
kwamba
mabadiliko
yoyote
yanayorudishwabaada ya kukamilika kwa uchunguzi.
(4) Wakati wa uchunguzi, afisa utekelezaji wa sheria
ataingiza:
(a) mbinu za kiufundi zilizotumika, muda na terehe
ya maombi;
(b) utambuzi wa mfumo wa kompyuta na maelezo
ya mabadiliko yaliyofanyika wakati wa
uchunguzi;

Select target paragraph3