61
No.14
Utoaji na
ukusanyaji wa
data nyendo
Utoaji na
ukusanyaji wa
maudhui katika
data
Sheria ya Makosa ya Mtandao
2015
(2) Mahakama inaweza, kwa maombi, kuongezea
muda amri chini ya kifungu cha 35 kwa muda ambao
itaona unafaa.
34.-(1) Endapo askari polisi mkuu wa kituo au afisa
utekelezaji wa sheria mwenye cheo cha askari mkuu wa
kituo anaridhika kuwa data kompyuta inahitajika kwa
madhumuni ya uchunguzi, afisa huyo anaweza kutoa amri
kimaandishi kwa ajili ya(a) utoaji au uwekaji kumbukumbu za taarifa za
kompyuta zinazohusiana na mawasilano maalum
kwa kipindi maalum; au
(b) kumruhusu na kumsaidia afisa utekelezaji wa
sheria kukusanya aukuwekea kumbukumbu data
hizo.
(2) Kwa madhumuni ya kifungu hiki “data nyendo”
maana yake ni taarifa:
(a) inayohusiana na mawasiliano kwa mfumo wa
kompyuta;
(b) iliyotolewa na mfumo wa kompyuta ambao ni
sehemu ya mlolongo wa mawasiliano; na
(c) inayoonyesha chanzo cha mawasiliano,njia
iliyotumika, muda,ukubwa, uelekeo na aina ya
huduma zinazoambatana nazo.
35. Endapo askari polisi mkuu wa kituo au afisa
utekelezaji wa sheria mwenye cheo cha askari mkuu wa
kituo ana sababu za msingi za kushuku au kuamini kuwa
yaliyomo kwenye mawasiliano ya kielektroniki yanahitajika
kwa madhumuni ya uchunguzi, anaweza kutoa amri ya:
(a) kukusanya, kurekodi, kuruhusu au kuisaidia
mamlaka husika kukusanya au kurekodi taarifa
zilizomo kwenye data inayohusishwa na
mawasiliano maalum yaliyotolewa kwa njia ya
mfumo wa kompyuta; au
(b) kukusanya au kurekodi data kwa kompyuta kwa njia ya
kiufundi.