No.14

Sheria ya Makosa ya Mtandao

2015

60

(iii)

shauri lolote lililopo mahakamani au
ambalo
linaweza
kufunguliwa
kuhusiana na uchunguzi wowote.
(6) Katika kifungu hiki “eneo” inajumuisha ardhi,
majengo au chombo cha usafiri baharini au ndege.
Utoaji data

32.-(1) Endapo data inahitajika kuwekwa wazi kwa
madhumuni ya uchunguzi wa kijinai au kuendeshwa kwa
kesi mahakamani, askari polisi mfawidhi wa kituo au afisa
mtekelezaji wa sheria mwenye cheo cha askari mkuu wa
kituo anaweza kutoa amri kwa mtu yeyote mwenye data
hiyo kumtaka kutoa data hiyo.
(2) Amri iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (1)
atapewa afisa utekelezaji sheria ambaye
ataiwasilisha kwa mtu huyo mwenye data.
(3) Endapo utoaji wa data chini ya kifungu kidogo
cha (1) hauwezekani, afisa utekelezaji sheria
anaweza kuiomba mahakama kutoa amri
inayotamka:
(a) mtu yeyote kuwasilisha data iliyoainishwa
ambayo mtu huyo anaimiliki au iliyo chini ya
uangalizi; au
(b) mtoa huduma anayetoa huduma zake,
kuwasilisha zinazohusu huduma hiyo zilizo
kwenye umiliki au uangalizi wake.
(4) Iwapo kitu chochote kinachohusiana na upelelezi
kinajumuisha data iliyohifadhiwa kwenye mfumo wa
kompyuta au kwenye kifaa, amri itachukuliwa kumtaka mtu
huyo kutoa au kuruhusu upatikanaji wa data hiyo katika
namna ambayo inasomeka na inayoweza kuondolewa.

Utunzaji data
wa dharura

33. (1) Endapo askari polisi Mkuu wa kituo au afisa
utekelezaji wa sheria anazo sababu za kuamini kuwa data
kompyuta ambayo inahitajika kwa madhumuni ya
uchunguzi inaweza kupotea au kubadilishwa, anaweza
kutoa amri itakayomtaka mtu mwenye uangalizi au umiliki
wa kifaa au data kompyuta hiyo kuitunza kwa kipindi
kisichozidi siku kumi na nne.

Select target paragraph3