59

No.14

Sheria ya Makosa ya Mtandao

2015

(iii) kuongeza wigo wa upekuzi au uwezo wa
kuingia kwenye mfumo mwingine iwapo
afisa utekelezaji wa sheria anayefanya
upekuzi ana sababu za kuaminika kuwa
data inayotafutwa, inatunzwa kwenye
mfumo mwingine wa kompyuta au sehemu
yake.
(2) Upekuzi chini ya kifungu hiki utafanyika kwa
mujibu wa sheria zinazosimamia masuala ya upekuzi na
ukamataji wa mali.
(3) Endapo kifaa au mfumo wa kompyuta
umeondolewa au hauingiliki kutokana na upekuzi au
ukamataji wa mali, afisa utekelezaji wa sheria, wakati wa
upekuzi na ukamataji wa mali au mara tu baada ya upekuzi(a) ataandaa orodha ya vitu vilivyokamatwa au
kufanywa visiingilike, muda ambao mali
ilikamatwa;
(b) atampatia nakala ya orodha ya mali
iliyokamatwa mtu anayemiliki au mwangalizi wa
mfumo husika wa kompyuta.
(4) Mtu anayemiliki au mwangalizi wa mfumo wa
kompyuta anaweza kumuomba afisa utekelezaji wa sheria
ruhusa ya kuingia au kudurufu taarifa zilizopo kwenye
mfumo wa kompyuta baada ya ukamataji wa mali.
(5) Bila ya kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha
(4), afisa utekelezaji wa sheria anaweza kukataa kuruhusu
kuingia kwenye mfumo au kudurufu taarifa iwapo ana
sababu za msingi za kuamini kuwa kuruhusu kuingia au
kudurufu taarifa(a) itakuwa ni kosa; au
(b) kutaathiri(i)
uchunguzi unaohusiana na upekuzi;
(ii)
upelelezi mwingine unaoendelea; au

Select target paragraph3