Na.14
Sheria ya Makosa ya Mtandao
2015
58
(c) limetendwa na Mtanzania; au
(d) limetendwa na Mtanzania anayeishi nje Jamhuri ya
Muungano
wa Tanzania,
endapo
kitendo
alichokitenda mtu huyo kingekuwa ni kosa chini ya
sheria ya nchi hiyo;
(e) limetendwa na mtu yeyote, bila kujali utaifa au
ukaazi wake au eneo husika, iwapo kosa
limefanyika(i) kwa kutumia mfumo wa kompyuta, kifaa
au data zilizoko ndani ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania; au
(ii) dhidi ya mfumo wa kompyuta, kifaa au
data au mtu aliye ndani ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
(2) Katika kifungu hiki, neno “mahakama” lina
maana ya mahakama yenye mamlaka.
SEHEMU YA NNE
UPEKUZI NA UKAMATAJI
Upekuzi na
ukamataji
31.-(1) Askari polisi mkuu wa kituo au afisa
utekelezaji wa sheria mwenye cheo cha askari mkuu wa
kituo, baada ya kuridhika kuwa kuna sababu za msingi
kushuku au kuamini kuwa mfumo wa kompyuta(a) unaweza kutumika kuthibitisha kosa; au
(b) unachukuliwa na mtu yeyote kutokana na kosaInaweza kutoa hati ya upekuzi itakayo muidhinisha afisa
utekelezaji wa sheria (i) kuingia kwenye eneo kwa lengo la
kupekua au kukamata kifaa au mfumo wa
kompyuta;
(ii) kuiwekea
ulinzi
data
kompyuta
iliyopatikana; au