57

No.14

Sheria ya Makosa ya Mtandao

2015

(e) njia zitakazotumika kuhifadhi au kutunza data au
taarifa kwenye miundombinu muhimu;
(f) mipango ya kudhibiti majanga iwapo kutatokea
uharibifu kwenye miundombinu muhimu au
sehemu yake;
(g) namna na utaratibu wa kuendesha ukaguzi
kwenye miundombinu muhimu yoyote;
(h) jambo jingine lolote ambalo ni muhimu kwa
ulinzi, usimamizi na udhibiti wa data na rasimali
nyingine kwenye miundombinu muhimu.
(3) Kwa madhumuni ya kifungu hiki,
“miundombinu muhimu ya TEHAMA” inajumuisha
mali, vifaa, mifumo ya kompyuta au mitandao
inayoshikika na isiyoshikika ambayo ina umuhimu
kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kiasi
kwamba kutokufanya kazi kwake kuna madhara ya
kiusalama, kiuchumi na kijamii.
Makosa
yanayohusu
miundombinu
muhimu ya
TEHAMA

29. Endapo mtu anatenda kosa chini ya Sheria hii
au sheria nyingine yoyote linalohusiana na miundombinu
muhimu, mtu huyo atakuwa ametenda kosa na akitiwa
hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shillingi milioni
mia moja au mara tatu ya hasara aliyoisababisha au kifungo
kisichopungua miaka mitano au vyote kwa pamoja.
SEHEMU YA TATU
MAMLAKA YA MAHAKAMA

Mamlaka ya
mahakama

30.-(1) Mahakama zitakuwa na uwezo wa kusikiliza
shauri lolote chini ya Sheria hii pale ambapo kosa au
sehemu ya kosa (a) limetendeka ndani ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania;
(b) limetendeka kwenye meli au ndege iliyosajiliwa
ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

Select target paragraph3