Na.14
Sheria ya Makosa ya Mtandao
2015
54
ametenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini
isiyopungua milioni tatu au kutumikia kifungo kwa muda
usiopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.
(2) Mtu ambaye kwa makusudi atazuia utekelezaji au
atashindwa kutekeleza amri iliyotolewa na sheria hii,
atakuwa ametenda kosa na atawajibika, iwapo atatiwa
hatiani, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au
kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka
mmoja au vyote kwa pamoja.
Unyanyasaji
kwa kupitia
mtandao
23.-(1)
Mtu
hataanzisha
au
kukadimisha
mawasiliano yoyote ya kielektroniki kwenda kwa mtu
yoyote kwa kutumia mfumo wa kompyuta, kwa lengo la,
kulazimisha, kutisha au kunyanyasa au kusababisha maudhi
ya hisia.
(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1)
atakuwa ametenda kosa na atawajibika, iwapo atatiwa
hatiani, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tano au
kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu
au vyote kwa pamoja.
Ukiukaji wa
haki bunifu
24.-(1) Mtu hatatumia mfumo wa kompyuta kwa
lengo la kukiuka haki bunifu zinazolindwa na sheria
nyingine yoyote.
(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1)
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika
iwapo ukiukaji (a) hauhusiani na masuala ya kibiashara, kulipa faini
isiyopungua shilingi milioni tano au kutumikia
kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu
au vyote kwa pamoja;
(b) unagusa masuala ya kibiashara, kulipa faini
isiyopungua shilingi milioni ishirini au