53
No.14
Sheria ya Makosa ya Mtandao
2015
Ujumbe
unaotumwa
bila ridhaa
20.-(1) Mtu ambaye kwa nia ya kutenda kosa
chini ya Sheria hii:(a) hataanzisha usambazaji wa ujumbe unaotumwa
bila ridhaa;
(b) hatarusha tena au kusambaza upya ujumbe
unaotumwa bila ridhaa;
(c) hataghushi ujumbe wa utambulisho na kutuma
bila ridhaa.
(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1)
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika
kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au mara tatu
ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au
yoyote iliyokubwa au kutumikia kifungo kwa kipindi
kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.
(3) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, “taarifa
zinazotumwa bila ridhaa” maana yake ni taarifa au data za
kielektroniki amabazo hazijaombwa na mpokeaji.
Ufichuaji wa
taarifa za
upelelezi
21.-(1) Mtu kwa makusudi na kunyume na sheria
hatatoa, taarifa yoyote inayohusiana na upelelezi wa jinai,
inayohitaji usiri.
(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1)
atakuwa ametenda kosa na atawajibika, iwapo atatiwa
hatiani, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni kumi au
kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu
au vyote kwa pamoja.
Kuzuia
upelelezi
22. Mtu ambaye kwa makusudi na kinyume cha
sheria ataharibu, atafuta, ataondoa, ataficha, atabadilisha au
ataifanya data kompyuta kukosa maana, kutofanya kazi au
kutotumika kwa lengo la kuharibu ushahidi au
kuchelewesha upelelezi atakuwa