55
No.14
Sheria ya Makosa ya Mtandao
2015
kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua
miaka mitano au vyote, kwa pamoja, pamoja na
kulipa fidia kwa mtu aliyeathirika na kosa husika
kiasi ambacho mahakama itaona kinafaa
Wakosaji
wakuu
25.-(1) Mtu yeyote ambaye(a) anafanya kitendo au anaacha kufanya kitendo
ambacho kiasi kwamba kutokutenda huko
kunasababisha kutendeka kwa kosa;
(b) anafanya au anaacha kufanya kitendo kwa
madhumuni ya kumwezesha au kumsaidia mtu
mwingine kutenda kosa;
(c) anamsaidia na kumwezesha mtu mwingine
kutenda kosa;
(d) anamshawishi au kumlipa mtu mwingine
kufanya kosa hilo,
atachukuliwa kuwa ameshiriki kutenda kosa na atashitakiwa
kama mtu aliyetenda kosa.
(2) Mtu anayemlipa mtu mwingine kufanya au
kutokufanya kitendo kwa kiasi ambapo, iwapo yeye
mwenyewe angefanya kitendo hicho au kutokutenda huko,
kitendo hicho kingepelekea kosa kufanyika kwa upande
wake na atakuwa na hatia kwa kosa la aina hiyo na
atawajibika kwa adhabu sawa kana kwamba yeye
mwenyewe angefanya kitendo hicho au kutokutenda huko.
Jaribio la
kufanya uhalifu
26.-(1) Endapo mtu anakusudia kutenda kosa
anaanza kutekeleza kusudio lake na anadhihirisha kusudio
lake kwa kitendo kinachoashiria kosa, isipokuwa hatekelezi
kusudio lake kwa kiasi cha kutenda kosa hilo, atachukuliwa
kuwa ametenda kosa hilo.
(2) Kwa madhumuni ya kifungu hiki haitakuwa
muhimu-