Na.14
Sheria ya Makosa ya Mtandao
2015
52
(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1)
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika
kulipa faini isiyopungua kiasi cha shilingi milioni tatu au
kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka
mmoja au vyote kwa pamoja.
Matusi ya
kibaguzi
18.-(1) Mtu hatamtukana au kumfedhehesha mtu
mwingine kwa kupitia mfumo wa kompyuta, kutokana na
sababu kuwa mtu huyo mwingine ni mmoja kati ya kundi
linalotambulika kwa tabaka, rangi, asili, utaifa, kabila au
dini fulani.
(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1)
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika
kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au kutumikia
kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote
kwa pamoja.
Mauaji ya
kimbari na
makosa dhidi
ya ubinadamu
19.-(1) Mtu hatachapisha au kusababisha
kuchapishwa kinyume na sheria vitu vinavyochochea,
kanusha, punguza au halalisha matendo yanasababisha
mauaji ya kimbari na makosa dhidi ya ubinadamu kwa
kupitia mfumo wa kompyuta.
(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1)
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika
kulipa faini isiyopungua shilingi milioni kumi au kutumikia
kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu au vyote
kwa pamoja.
(3) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, tafsiri ya
“mauaji ya kimbari” itakuwa na maana kama ilivyo
tafsiriwa katika Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu
wa Mauaji ya Kimbari wa mwaka 1948.