51

No.14

Sheria ya Makosa ya Mtandao

2015

(a) ponografia, kulipa faini isiyopungua shilingi
milioni ishirini au kutumikia kifungo kwa
kipindi kisichopungua miaka saba au vyote kwa
pamoja; au
(b) ponografia iliyo ya kiasherati au chafu, kulipa
faini isiyopungua shilingi milioni thelathini au
kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua
miaka kumi au vyote kwa pamoja.
Makosa
yanayohusiana
na utambuzi

15.-(1) Mtu hatajifanya kuwa mtu mwingine kwa
kutumia mfumo wa kompyuta.
(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1)
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika
kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tano au mara tatu
ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au
yoyote iliyokubwa au kutumikia kifungo kwa kipindi
kisichopungua miaka saba au vyote kwa pamoja.

Kutoa taarifa za
uongo

16. Mtu atakayechapisha taarifa au data katika picha,
maandishi, alama au katika namna nyingine yoyote katika
mfumo wa kompyuta, akijua kwamba taarifa au data ni za
uongo, zinapotosha, zisizo sahihi, na kwa lengo la
kudhalilisha, kutishia, kutusi au kwa naamna nyingine
kudanganya umma au kuchochea utendaji wa kosa, atakuwa
ametenda kosa, na akipatikana na hatia atalipa faini
isiyopungua shilingi milioni tano au kutumikia kidungo
kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja.

Ubaguzi

17.-(1) Mtu, kwa kutumia mfumo wa kompyuta(a) hatazalisha vitu vya kibaguzi kwa madhumuni ya
kuvisambaza;
(b) hatatoa au kuwezesha kupatikana vitu vya
kibaguzi ; au
(c) hatarusha au kusambaza vitu vya kibaguzi.

Select target paragraph3