Na.14
Sheria ya Makosa ya Mtandao
2015
50
(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1)
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika,
kulipa faini isiyopungua shilingi milioni ishirini au mara
tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria,
au yoyote iliyokubwa au kutumikia kifungo kwa kipindi
kisichopungua miaka saba au vyote kwa pamoja.
Ponografia za
watoto
13.-(1) Mtu yeyote(a) hatachapisha ponografia za watoto kwa kupitia
mfumo wa kompyuta; au
(b) hatatoa au hatawezesha upatikanaji au
kuonyeshwa kwa ponografia za watoto kwa
kupitia mfumo wa kompyuta.
(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1)
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika
kulipa faini isiyopungua shilingi milioni hamsini au mara
tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria,
au yoyote iliyokubwa au kutumikia kifungo kwa kipindi
kisichopungua miaka saba au vyote kwa pamoja.
(3) Mtu aliyetiwa hatiani kwa kosa chini ya kifungu
hiki, pamoja na adhabu nyingine yoyote, anaweza kuamriwa
kumlipa fidia mtu ambaye ameathirika na kosa hilo.
Ponografia
14.-(1) Mtu hatachapisha au kusababisha
kuchapishwa kupitia katika mfumo wa kompyuta(a) ponografia; au
(b) ponografia yoyote iliyo ya kiasherati au chafu.
(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1)
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika,
iwapo ni uchapishaji kuhusiana na-