49
No.14
Sheria ya Makosa ya Mtandao
2015
mtu yoyote kuingilia mfumo wa kompyuta au
sehemu yake kwa lengo la kutenda kosa.
(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1)
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika,
kulipa faini isiyopungua shilingi milioni kumi au mara tatu
ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au
yoyote iliyokubwa au kutumikia kifungo kwa kipindi
kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja.
Kughushi
kunakohusiana
na masuala ya
kompyuta
11.-(1)
Mtu
hataingiza,
hatabadilisha,
hatachelewesha, hatasambaza au hatafuta data kompyuta
iliyoghushiwa kwa lengo la kutaka itumike bila kujali kama
taarifa hiyo inasomeka au haisomeki.
(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1)
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika,
kulipa faini isiyopungua shilingi milioni ishirini au mara
tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria,
au yoyote iliyokubwa au kutumikia kifungo kwa kipindi
kisichopungua miaka saba au vyote kwa pamoja.
Udanganyifu
unaohusiana na
kompyuta
12.-(1) Mtu hatasababisha upotevu kwa mali ya mtu
mwingine kwa(a) kuongeza, kubadilisha, kufuta, kuchelewesha
kusambaza au kuzuia data kompyuta; au
(b) kuingilia utendaji kazi wa mfumo wa kompyuta,
kwa udanganyifu au uongo kwa lengo la kujipatia bila haki
manufaa ya kiuchumi.