Na.13

Sheria ya Miamala ya Kielektroniki

2015

22

(2)
Endapo mtoa huduma anashindwa kutekeleza
agizo ndani ya muda uliotajwa chini ya kifungu kidogo cha
(1), mtumiaji anaweza kufuta makubaliano kwa kutoa taarifa
ya siku saba.
(3)
Endapo mtoa huduma anashindwa kutekeleza
mkataba kutokana na sababu kuwa bidhaa au huduma
zilizoagizwa hazipatikani, mtoa huduma, ndani ya siku
thelathini, atamtaarifu mtumiaji na mtoa huduma atarudisha
malipo yoyote ambayo yatakuwa yamefanyika.
Haki ya
usitishaji

30.-(1)
Bila ya kuathiri sheria nyingine yoyote,
mtumiaji, anaweza ndani ya siku saba au muda mwingine
zaidi uliokubalika ndani ya mkataba, baada ya kupokea
bidhaa au kukamilika kwa makubaliano na mtumiaji
hajapokea faida yoyote kutokana na miamala, huo kufuta
makubaliano hayo kwa ajili ya usambazaji wa bidhaa au
utolewaji wa huduma.
(2)
Endapo mtumiaji anafuta mkataba chini ya
kifungu kidogo cha (1), atalipa gharama zote za moja kwa
moja za kurudisha bidhaa.
(3) Endapo mtumiaji amelipia bidhaa au huduma
kabla ya kutekeleza haki iliyotolewa chini ya kifungu kidogo
cha (1), atastahili kurudishiwa fedha.
(4) Fedha itakayotolewa chini ya kifungu kidogo cha
(3) italipwa ndani ya siku thelathini baada ya tarehe ya
kufutwa kwa muamala.
(5)
Kifungu hiki hakitatumika kwa miamala ya
kielektroniki(a) kwa ajili ya huduma za kifedha;
(b) kwa njia ya mnada;
(c) kwa usambazaji wa vyakula, vinywaji au bidhaa
nyingine zilizokusudiwea kwa ajili ya matumizi ya
kila siku;

52

Select target paragraph3