23

Na.13

Sheria ya Miamala ya Kielektroniki

2015

(d) kwa huduma zilizotokana na idhini ya mtumiaji
kabla ya kupita kwa muda wa siku saba;
(e) iwapo bei ya kusambaza bidhaa au huduma
inategemea mfumuko wa bei katika masoko ya
fedha na ambayo hayawezi kudhibitiwa na
mtumiaji;
(f) iwapo bidhaa:
(i)
zimetengenezwa ili kukidhi matakwa
ya mtumiaji;
(ii)
zimetengenezwa maalum kwa ajili
maalum;
(iii) kutokana na hali yake, haziwezi
kurudishwa; au
(iv)
zina uwezekano wa kuharibika au
kupitwa na muda wa matumizi haraka;
(g) iwapo rekodi za kusikiliza au za video au
programu za kompyuta zilipakuliwa au
kuondolewa lakiri na mtumiaji;
(h) kwa ajili ya uuzaji wa magazeti, makala, majarida
na vitabu;
(i) kwa ajili ya kutolewa kwa huduma za michezo ya
kubahatisha au bahati nasibu;
(j) kwa ajili ya michezo ya kubahatisha inayofanyika
kwa kupitia mtandao;
(k) kwa ajili ya kutolea huduma za malazi, usafiri na
chakula; na
(l) kwa kadri ambavyo Waziri anaweza kwa tangazo
litakalochapishwa kwenye Gazeti la Serikali,
kuanzisha miamala mingine yoyote.
(6) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, “gharama za
moja kwa moja” maana yake ni gharama zilizoingiwa na
zinajumuisha gharama za usafiri au kutumia wakati wa
kurudisha bidhaa au huduma, isipokuwa haitajumuisha
gharama zozote za upakiaji au usambazaji.

53

Select target paragraph3