21

Na.13

Sheria ya Miamala ya Kielektroniki

2015

SEHEMU YA SITA
ULINZI KWA MTUMIAJI
Wajibu wa
watoa
huduma kwa
watumiaji
wa mtandao

28-(1) Mtoa huduma anayeuza bidhaa au huduma
kwa ajili ya mauzo, kukodisha au kwa ajili ya kubadilishana
kwa njia ya kielektroniki, atatoa taarifa zifuatazo kwa
watumiaji(a) jina kamili, hadi ya kisheria na eneo la biashara;
(b) maelezo yanayohusu anuwani yake kupatikana
kwake zikijumuisha anuani ya makazi, nambari za
simu na anuani ya barua pepe;
(c) maelezo kamili ya bidhaa au huduma
zinazotolewa;
(d) bei ya bidhaa au huduma hiyo;
(e) taarifa inayohusu malipo yatakayofanywa kwa
mujibu wa sheria nyingine; na
(f) taarifa nyingine yoyote muhimu.
(2)
Kabla ya mtumiaji hajatoa maombi yake ya
bidhaa au huduma, mtoa huduma atatoa nafasi kwa mtumiaji
ya (a) kufanya mapitio ya muamala mzima wa
kielektroniki;
(b) kurekebisha makosa yoyote; na
(c) kujitoa kwenye muamala huo.
(3) Endapo mtoa huduma anakiuka masharti ya
kifungu hiki, mtumiaji anaweza, ndani ya siku kumi na nne
baada ya kupokea bidhaa au huduma, kufuta muamala.

Muda kwa
ajili ya
kutekeleza
agizo

29.-(1) Isipokuwa kama wahusika wamekubaliana
vinginevyo, mtoa huduma atatekeleza agizo ndani ya siku
thelathini kutokea siku ambayo mtoa huduma amepokea
maombi ya bidhaa au huduma.

51

Select target paragraph3