Na.13

Sheria ya Miamala ya Kielektroniki

2015

20

unaoingiliana hautoi nafasi kwa mtu kurekebisha kosa hilo ,
mtu huyo atakuwa na haki ya kuondoa mawasiliano hayo ya
kielektroniki ambamo ndani yake amefanya kosa la
kiuingizaji, wapo(a) anamtaarifu mhusika wa upande wa pili kuhusiana
na kosa hilo haraka iwezekanavyo baada ya
kugundua kosa hilo na anakusudia kusitisha
mkataba au kurekebisha kosa la kiuingizaji ;
(b) anachukua hatua madhubuti kutekeleza maelekezo
yaliyotolewa na upande wa pili kurudisha bidhaa
au huduma alizopokea kutokana na kutendeka kwa
kosa hilo au kuharibu bidhaa au huduma au
kurekebisha kosa hilo; na
(c) hajatumia au kupokea faida yoyote au thamani ya
bidhaa au huduma hiyo au kosa la kiuingizaji
kutoka kwa mhusika wa upande wa pili.
(4) Mtu ambaye ameshalipia bidhaa au huduma kabla
ya kutekeleza haki iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha
(1), atastahili kurudishiwa malipo yake yote ndani ya siku
thelathini baada ya kufutwa kwa muamala.
(5)
Hakuna kitu chochote katika kifungu hiki
kitakachoathiri matumizi ya sheria yoyote inayosimamia
masuala yatokanayo na makosa yaliyofanywa wakati wa
ufugwaji au utekelezaji wa aina ya mkataba huo mbali na kosa
linalo husiana na uingizaji linatokea katika mazingira ya
kifungu kidogo cha (3).
Mnada
kupitia
mtandao

27.
Endapo sheria inahitaji mkataba wa mauzo,
utekelezwe kwa njia ya mnada, masharti ya “nyundo
kugongwa” yatakuwa yamezingatiwa katika mnada
utakaofanyika kupitia mtandao kwa kutumia muda ambao
mawasiliano ya kielektroniki yalipokelewa kama kigezo cha
ukomo wa muda kama njia ya kumchagua mzabuni wa
mwisho.

50

Select target paragraph3