13

Na.13

Sheria ya Miamala ya Kielektroniki

2015

Malipo ya
fedha na utoaji
wa stakabadhi
kwa njia ya
kielektroniki

15. Endapo sheria inahitaji(a) malipo kufanyika, masharti hayo yatakuwa
yametekelezwa
iwapo
malipo
yatakuwa
yamefanyika kwa njia ya kielektroniki na kukidhi
masharti yoyote yaliyotolewa na sheria nyingine
husika; na
(b) utoaji wa stakabadhi yoyote ya malipo, masharti
hayo yatakuwa yametekelezwa iwapo stakabadhi
hiyo itakuwa katika mfumo wa ujumbe wa
kielektroniki na ujumbe kusomeka na unaeleweka
kiasi kwamba unaweza kutumika katika rejea.

Uchapishaji wa
nyaraka

16.
Endapo sheria inahitaji nyaraka kuchapishwa
kwenye Gazeti la Serikali, masharti hayo yatakuwa
yametimizwa iwapo nyaraka hiyo itachapishwa kwenye
Gazeti la Serikali la kielektroniki.

Nyaraka katika
mfumo wa
kielektronniki
haitakuwa
lazima

17.
Sheria hii haitatoa haki kwa mtu yeyote
kushinikiza taasisi ya yoyote ya umma kushughulikia nyaraka
yoyote kielektroniki.

SEHEMU YA NNE
KUKUBALIKA NA UZITO WA USHAHIDI WA UJUMBE WA DATA
Kukubalika
kwa ujumbe wa
data

18.-(1)
Katika mwenendo wa shauri lolote la
kisheria, kanuni za ushahidi kitakacho tumika ili kukataa
kukubalika kwa ushahidi wa ujumbe data kwa kigezo kwamba
ni ujumbe data.
(2) Katika kuamua kukubalika na uzito wa ushahidi
wa ujumbe data, yafuatayo yatazingatiwa(a) kuaminika kwa namna ambayo ujumbe data
umetengenezwa, umehifadhiwa au umewasilishwa;
(b) kuaminika kwa namna ambayo uadilifu wa ujumbe
data ulivyohifadhiwa;

43

Select target paragraph3