Na.13

Sheria ya Miamala ya Kielektroniki

2015

14

(c) namna ambayo chanzo cha ujumbe data
kimetambuliwa;
(d) vigezo vingine vyovyote vinavyofaa katika
kutathmini uzito wa ushahidi huo.
(3)
Uhalali wa kumbukumbu za mfumo wa
kielektroniki ambamo kumbukumbu ya kielektroniki
inanukuliwa au kutunzwa, iwapo hakuna ushahidi kinyume
na, utachukuliwa kuwa(a) iwapo kuna ushahidi unaothibitisha ukweli kuwa
katika muda wote, mfumo wa kompyuta au kifaa
kama hicho kilikuwa kinafanya kazi vizuri au
iwapo hakikuwa kinafanya kazi vizuri, kitendo cha
kutokufanya kazi kwake vizuri hakukuathiri
uadilifu wa kumbukumbu ya kielelektroniki na
hakuna sababu nyingine za msingi kushuku uhalali
wa kumbukumbu za mfumo wa kielektroniki;
(b) iwapo inabainika kwamba kumbukumbu ya
kielektroniki ilirekodiwa au kuhifadhiwa na
mhusika katika shauri ambaye ana maslahi tofauti
na mhusika wa upande unaotaka kuutumia
ushahidi huo; au
(c) imebainika kuwa kumbukumbu ya kielektroniki
ilirekodiwa au kuhifadhiwa katika utendaji kazi wa
kawaida na mtu ambaye si mhusika katika shauri
na ambaye hakurekodi au kuhifadhi kumbukumbu
chini ya uangalizi wa mhusika wa upande
unaotaka kuutumia ushahidi huo.
(4) Kwa madhumuni ya kuamua iwapo kumbukumbu
ya kielektroniki inakubalika chini ya kifungu hiki, ushahidi
unaweza kutolewa kuhusiana na kiwango chochote
kilichowekwa, taratibu, mila au uzoefu kuhusiana na namna
ambavyo

44

Select target paragraph3