Na.13
Sheria ya Miamala ya Kielektroniki
2015
12
(a) namna na mfumo ambao muamala wa
kielektroniki unaweza kufanyika;
(b) aina ya saini ya kielektroniki inayohitajika, pale
ambapo muamala wa kielektroniki unatakiwa
kusainiwa;
(c) namna na mfumo ambao saini ya kielektroniki
inaweza kuambatanishwa au kuhusishwa na
muamala wa kielektroniki;
(d) mchakato wa udhibiti na taratibu za kuhakikisha
uadilifu usalama na usiri wa taarifa;
(e) utambulisho au utaratibu utakaozingatiwa na mtoa
huduma aliyeidhinishwa kwa ajili ya kuwasilisha
muamala wa kielektroniki;
(f) mchakato wa udhibiti na utaratibu utakao
hakikisha uadilifu wa kutosha, usalama na usiri wa
muamala
wa
kielektroniki
au
malipo
yakielektroniki; na
(g) masharti
mengine
kwa
yoyote
ambayo
yanahusiana na miamala ya kielektroniki.
(5) Bila kujali kifungu kidogo cha (4), taasisi yoyote
iliyoidhinishwa, inaweza kutumia taratibu nyingine za
uthibitishaji.
Uwasilishaji
wa nyaraka
kwa njia ya
kielektroniki
14.-(1) Endapo sheria inahitaji nyaraka kuwasilishwa,
masharti hayo yatakuwa yametimizwa iwapo nyaraka hiyo
imewasilishwa kwa njia ya kielektroniki.
(2) Kifungu kidogo cha (1) kitatumika pale ambapo
kuna mfumo wa kuandaa taarifa ambao unaweza(a) kutambua chanzo, mwelekeo, muda na tarehe ya
kutowasilishwa, kutuma na kupokea kwa taarifa;
(b) kuthibitisha kupokewa kwa nyaraka.
42