Na.14

Sheria ya Makosa ya Mtandao

2015

56

(a) isipokuwa kwa kiasi cha adhabu, iwapo(i) mkosaji anatenda yote ambayo ni
muhimu kwa utendaji wa kosa; au
(ii) utekelezaji wa kusudio lake kwa
ukamilifu unazuiliwa na mazingira
ambayo hayaingiliani na kusudio lake;
au
(iii) anaacha kutekeleza kusudio lake kwa
hiari yake mwenyewe;
(b) kutokana na sababu za mazingira yasiyojulikana
kwa mhalifu, haiwezekani kutenda kosa.
(3) Mtu yeyote anayejaribu kutenda kosa chini ya
Sheria hii atakua ametenda kosa na akitiwa hatiani
atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni moja
au kifungo kwa kipindi kisichopungua miezi sita au vyote
kwa pamoja.
Kula njama ya
kutenda kosa

27. Mtu yeyote anayekula njama na mtu mwingine
kutenda kosa chini ya Sheria hii, anatenda kosa na iwapo
atatiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi
milioni moja au kutumikia kifungo kwa kipindi
kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.

Ulinzi wa
miundombinu
muhimu ya
TEHAMA

28.-(1) Waziri anaweza, kwa amri itakayochapishwa
kwenye Gazeti la Serikali kuainisha mifumo ya kompyuta
kama miundombinu muhimu.
(2) Amri iliyorejewa chini ya kifungu kidogo cha (1)
inaweza kuainisha miongozo au taratibu zinazohusu (a) usajili, ulinzi au utunzaji wa miundombinu
muhimu;
(b) usimamizi wa jumla wa miundombinu muhimu;
(c) kuingia, kuhamisha na kudhibiti data kwenye
miundombinu muhimu;
(d) uwepo wa audilifu au uhalali wa data au taarifa
zilizo katika miundombinu muhimu;

Select target paragraph3