Na.13
Sheria ya Miamala ya Kielektroniki
2015
6
kwenda kwenye mfumo mwingine;
“mawasiliano ya kielektroniki” manta yake ni uhamishaji
wowote wa alama, mawimbi au data zozote za
kompyuta za aina yoyote zilizosafirishwa kwa
mkupuo au sehemu kwa njia ya waya, redio,
sumaku, picha za kielektroniki, picha za kioo au kwa
njia nyingine yoyote zinazofanana na hiyo;
“Gazeti la Serikali la kielektroniki” maana yake ni Gazeti la
Serikali linalorejewa kwenye kifungu cha 16;
“kumbukumbu ya
kielektroniki” maana yake ni
kumbukumbu iliyotunzwa kwa njia ya kielektroniki;
“saini ya kielektroniki” maana yake ni data, ikijumuisha,
sauti ya
kielektroniki, alama au mchakato
uliofanyika au kutumika katika kumtambua
mhusika, ili kuashiria ridhaa au kusudio lake
kuhusiana na taarifa iliyoko katika mawasiliano ya
kielektroniki na ambayo imeambatanishwa kwenye
au kimantiki inahusiana na mawasilano ya
kielektroniki;
“muamala wa kielektroniki” maana yake ni muamala,
kitendo au fungo la miamala ama ya kibiashara au
yasiyo ya kibiashara ambayo inafanyika kwa njia
ya kielektroniki;
“mfumo wa ujumbe unaojiendesha” maana yake ni mfumo
unaojiendesha wenyewe au programu nyingine
36