25

Na.13

Sheria ya Miamala ya Kielektroniki

2015

(d) fursa ya kujitoa imetolewa na mtoa taarifa kwenda
kwa mlengwa kwa kila ujumbe utakaotumwa.
(3) Mtuma taarifa atayayekiuka masharti ya kifungu
hiki atakuwa ametenda kosa na atawajibika, pale atakapotiwa
hatiani, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni kumi au
kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja
au vyote kwa pamoja.
SEHEMU YA SABA
WATOA HUDUMA ZA KRAIPTOGRAFIA NA UIDHINISHAJI
Huduma za
kraiptografia
na
uidhinishaji

33. Waziri anaweza, kwa taarifa itakayochapishwa
kwenye Gazeti la Serikali, kuteua taasisi ya kiserikali chini ya
Wizara yenye dhamana na Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano kuwa mdhibiti wa Huduma za Kraiptografia na
Uidhinishaji.

Majukumu
ya mdhibiti

34. Majukumu ya mdhibiti huyo yatakuwa ni(a) kutoa leseni na kusimamia huduma za
kraiptografia na uidhinishaji;
(b) kuainisha
viwango
vya
kiusalama
vya
kraiptografia na saini za za kielektroniki;
(c) kuamua viwango vitakavyozingatiwa na mamlaka
za uidhinishaji;
(d) kuweka na kutunza rejesta ya watoa huduma wa
huduma za kraiptografia na uidhinishaji; na
(e) kufanya vitu vingine vyovyote ambavyo ni
muhimu kwa utekelezaji wa masharti ya Sehemu
hii.

Maombi ya
usajili

35.
(1) Mtu anayekusudia kutoa huduma za
kraiptografia au uidhinishaji atawasilisha maombi yake kwa
mdhibiti .
(2) Maombi yaliyofanywa chini ya kifungu kidogo cha
(1) yatakuwa na maelezo yafuatayo:

55

Select target paragraph3