7
Na.13
Sheria ya Miamala ya Kielektroniki
2015
iliyoandaliwa awali, inayotumika kuanzishia
kitendo, kujibu mawasiliano ya kielektroniki au
kuzalisha kazi nyingine kwa ukamilifu au kwa
sehemu pasipo kurejea au kuingiliwa na mhusika
kila wakati kitendo kinapofanywa au jibu
linapotolewa na mfumo;
“Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana na
masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano;
“mtuma taarifa” maana yake ni mtu ambaye kutoka kwake
mawasiliano ya kielektroniki yanadaiwa kuwa
aliyatuma au kuyayazalisha;
“sehemu ya biashara” maana yake ni sehemu yoyote
ambayo mhusika anatunza ana mahala pa kuendesha
shughuli ya kiuchumi mbali ya shughuli ya muda ya
uuazaji wa bidhaa au huduma katika eneo maalum.
SEHEMU YA PILI
UTAMBUZI NA MATOKEO YA MIAMALA YA
KIELEKTRONIKI
Kutambulika
kwa ujumbe
wa data
4. Ujumbe wa data hautakataliwa nguvu ya kisheria,
uhalali au ktumuika kwake kwa sababu ya kuwa
umetengenezwa katika mfumo wa kielektroniki.
Uhalali wa
muamala wa
kielektroniki
5.-(1) Endapo sheria inahitaji taarifa au muamala
kuwa katika namna iliyoainishwa isiyo ya kielektroniki au
kimaandishi, masharti hayo yatakuwa yametimizwa na taarifa
au muamala wa kielektroniki ambayo(a) imewekwa katika namna sawa au inayokaribiana
na namna maalum isiyo ya kielektroniki;
(b) inaweza kufikiwa na mtu mwingine kwa ajili ya
rejea; na
37