Matumizi

Na.13

Tafsiri

2. Isipokuwa kwa Sehemu ya Tatu, Sheria hii
itatumika Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Sheria ya Miamala ya Kielektroniki

2015

5

3. Katika Sheria hii, isipokuwa kama muktadha
utahitaji vinginevyo“kuingia” kuhusiana na mfumo wowote wa kompyuta
maana yake ni kupata fursa ya kuingia, kutoa
kuelekeza, kuwasiliana na, kuhifadhi data katika,
kupokea data kutoka katika au vinginevyo kutumia
rasilimali zozote za mfumo wa kompyuta au
mtandao au mfumo wa kifaa cha kutunzia data ;
“mlengwa” maana yake ni mtu au mhusikaambaye
amedhaminiwa na mtumaji taarifa kupokea
mawasiliano
ya
kielektroniki,
isipokuwa
haitajumuisha mtu anayetenda kama mtu kati
kuhusiana na mawasiliano ya kielektroniki;
“mfumo wa kompyuta” maana yake ni kifaa au mjumuiko
wa vifaa, ikijumuisha mtandao, vifaa vya kwingiza
na kutoa vinavyoweza kutumika pamoja na majalada
ya nje ambayo yana programu za kompyuta,
maelezo yakielektroniki, data zinazoingia na
zinazotoka ambazo zinaleta mantiki, uhifadhi wa
data za namba na udhibiti wa mawasiliano
yanayorejea;
“mtumiaji” maana yake ni mtu yeyote ambaye anayeingia
au anayekusudia kuingia katika muamala wa
kielektroniki na mtoa huduma akiwa kama mtumiaji
wa mwisho wa bidhaa au huduma zinazotolewa na
mtoa huduma;
“kraiptografia” maana yake ni utaalam wa kulinda taarifa
kwa
kuzibadilisha
kuwa
kwenye
mfumo
usiosomeka;
“data” maana yake ni taarifa yoyote iliyowasilishwa kwa
njia ya kielektroniki;
“ujumbe wa data” maana yake ni ujumbe uliyotengenezwa,
uliyowasilishwa, uliyopokelewa au kutunzwa kwa
njia ya kielektroniki, kwa simaku au njia nyingine

34

Select target paragraph3