Na.13

Sheria ya Miamala ya Kielektroniki

2015

16

(2) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo cha (1),
uadilifu wa taarifa iliyoko kwenye nyaraka utakuwa
umezingatiwa iwapo taarifa itabaki kuwa kamili na
haijabadilishwa, isipokuwa kwa:
(a) kuweka nyongeza ya uthibitisho wowote; au
(b) mabadiliko yoyote ya msingi, ambayo yanatokea
wakati wa kufanya mawasiliano ya kawaida,
utunzaji au uwekaji wazi.
SEHEMU YA TANO
UTAMBUZI WA MIKATABA YA KIELEKTRONIKI
Utambuzi wa
mikataba ya
kielektroniki

21.-(1) Kwa madhumuni ya kuondoa shaka, mkataba
unaweza kuandaliwa kwa njia ya kieleketroniki isipokuwa
kama imekubaliwa vinginevyo na wahusika.
(2) Endapo kumbukumbu za kielektroniki zinatumika
katika kuandaa mkataba, mkataba huo hautapoteza nguvu ya
kisheria au uwezo wa kutekelezwa kutokana na sababu kuwa
kumbukumbu za kielektroniki zilitumika kwa madhumuni
hayo.

Muda wa
kutuma na
kupokea
mawasiliano
ya
kielektroniki

22.-(1) Taarifa iliyoko kwenye mfumo wa
kielektroniki itachukuliwa kuwa imetumwa pale inapoingia
kwenye mfumo wa mawasiliano ulio nje ya uwezo wa chanzo
cha taarifa au mtu ambaye aliituma taarifa hiyo ya
kielektroniki kwa niaba ya chanzo.
(2) Endapo au mlengwa wa taarifa wapo kwenye
mfumo mmoja wa mawasiliano ya kielektroniki, taarifa ya
kielektroniki itachukuliwa kuwaimewasilishwa pale ambapo
mlengwa anaweza kupata taarifa hiyo.
(3) Endapo mlengwa ametenga mfumo wa kompyuta
kwa madhumuni ya kupokea mawasiliano ya kielektroniki,
taarifa hiyo itachukuliwa kuwa imepokelewa wakati
mawasiliano ya kielektroniki yanaingia kwenye mfumo wa
mawasiliano uliotengwa.

46

Select target paragraph3