Na.13

Sheria ya Miamala ya Kielektroniki

2015

24

Taarifa zitakazo
tolewa katika
mawasiliano ya
kielektroniki

31.-(1)
Mtu anayeuza bidhaa au huduma za
mawasiliano ya kielektroniki atampatia mlengwa –
(a) utambulisho wa chanzo cha mawasiliano na
maelezo kuhusiana na anuwani yake;
(b) chombo halali cha utekelezaji ambacho kitatoa
nafasi ya mtu kuamua kutokuendelea kupokea
mawasiliano katika siku za mbele; na
(c) maelezo kuhusiana na chanzo ambacho kutoka
kweke chanzo cha mawasiliano kilipata taarifa
binafsi za mlengwa.

Bidhaa, huduma
au mawasiliano
ambayo
hayajaombwa

32.-(1)
Mtu hatatuma mawasiliano ya kibiashara
yanayphusu bidhaa au huduma ambazo hazijaombwa na
mlengwa, isipokuwa kama(a) mtumiaji anaridhia mawasiliano hayo;
(b) mwanzoni mwa mawasiliano, mawasiliano hayo
yanaweka wazi utambulisho wa mtumaji na
madhumuni ya mawasiliano; au
(c) mawasiliano hayo yanaweka utaratibu wa kukataa
mawasiliano hayo siku zijazo.
(2) Masharti ya mtu kuridhia ama kutokuridhia
yatachukuliwa kuwa yametimizwa iwapo(a) anuwani ya mlengwa wa mawasiliano na taarifa
nyingine binafsi ambayo ilikusanywa na mtuma
taarifa wakati wa mauzo au majadiliano kwa ajili
ya mauzo;
(b) mtuma taarifa anatuma matangazo ya biashara
yanayohusiana bidhaa au huduma zinazofanana
kwa mlengwa;
(c) mtoa taarifa ametoa nafasi kwa mlengwa fursa ya
kujitoa na kufanya hivyo; na

54

Select target paragraph3