19
Na.13
Sheria ya Miamala ya Kielektroniki
2015
(ii)
pale ambapo hakuna muamala, sehemu
yake aliyoizoea kwa ajili ya biashara.
(4)
Iwapo kampuni hodhi haina sehemu ya
biashara, sehemu ya biashara itakuwa ni anwani ya kibiashara
ya kampuni hiyo au sehemu ilisajiliwa au kuanzishwa
kisheria.
(5)
Kifungu hiki kitatumika bila kujali kwamba
sehemu ambapo mfumo wa kompyuta unaowiana na
unawezesha kupatikana kwa anwani ya kielektroniki upo
katika sehemu iliyotofauti na sehemu ambapo mawasiliano
yakielektroniki yatachukuliwa kuwa yamepelekwa au
kupokelewa.
Muda na mahali
ambapo mkataba
umefungwa
25.-(1) Endapo wahusika wanaingia kwenye mkataba
kwa njia ya kielektroniki, mkataba huo utakuwa umefungwa
kwa muda huo na sehemu ambayo mawasiliano ya
makubaliano yalipokelewa.
(2) Mapendekezo ya mkataba yaliyo katika mfumo
wa kielektroniki yatakuwa na nguvu katika muda ambao
yatapokelewa na mpokea mapendekezo.
Mikataba kupitia
mifumo
inayojiendesha
26.-(1) Mkataba ulioingiwa kwa njia ya mwingiliano
kati ya mfumo unayojiendesha wenyewe na mtu binafsi au
mifumo yenyewe, haitapoteza nguvu ya kisheria kutokana na
sababu kuwa hakuna mtu aliyefanya mapitio ya matendo ya
kila mmoja wao yaliyotendwa kwa mifumo kuingiliana.
(2)
Mfumo unaojiendesha wenyewe utatoa nafasi
kwa mtu kurekebisha kosa lolote la kiuingizaji wa taarifa
lililofanywa katika mawasiliano ya kielektroniki baina ya
mifumo inayoingiliana na mhusika wa upande wa pili.
(3) Endapo mtu anafanya kosa la kiuingizaji kwenye
mawasiliano ya kielektroniki baina ya mifumo unaojiendesha
wenyewe na mhusika wa upande wa pili na mfumo huo
49