Na.13

Sheria ya Miamala ya Kielektroniki

2015

18

kawaida, basi chanzo cha mawasiliano kinaweza
kutoa taarifa kwenda kwa mlengwa ikielezea kuwa
hakuna uthibitisho aliyopokea na ikiainisha muda
wa kawaida ambao kwayo uthibitisho wa taarifa
unatakiwa kuwa umepokelewa naye; au
(b) ndani ya ukomo wa muda uliotajwa, anaweza,
baada ya kutoa taarifa kwa mlengwa, kuyachukulia
mawasiliano hayo ya kielektroniki kama vile
hayakuwahi kutumwa kabisa.
Mahali pa
kutuma na
kupokea
mawasiliano
ya
kielektroniki

24.-(1) Isipokuwa kama imekubalika vinginevyo kati
ya chanzo cha mawasiliano na mlengwa, mawasiliano ya
kielektroniki yatachukuliwa kuwa yametumwa kwenye
sehemu ambapo chanzo cha mawasiliano kinaendesha
biashara yake na yatachukuliwa yamepokelewa katika sehemu
ambayo mlengwa anaendesha biashara yake.
(2) Kifungu kidogo cha (1) kitatumika(a) hata kama chanzo cha taarifa au mlengwa
hakuwepo katika sehemu yake ya kawaida ya
biashara; na
(b) kuamua sehemu ambapo mkataba uliingiwa kwa
madhumuni ya kulipa kodi.
(3)
Kwa madhumuni ya kifungu kidogo cha (1),
iwapo chanzo cha mawasliano au mlengwa (a) ana sehemu ya biashara zaidi ya moja, sehemu ya
biashara itakuwa ni:
(i)
ile ambayo inahusiana kwa karibu zaidi
na muamala husika kwa kuzingatia
mazingira yanayojulikana
au ya
kufikiriwa na wahusika katika muda
wowote kabla au wakati wa kufikia
makubaliano ya mkataba; au

48

Select target paragraph3