17

Na.13

Sheria ya Miamala ya Kielektroniki

2015

(4) Endapo mawasiliano ya kielektroniki yanatumwa
kwenye mfumo wa mawasiliano wa mlengwa ambao ni
tofauti na mfumo wa kompyutauliotengwa, taarifa hiyo
itachukuliwa kuwa imewasilishwa(a) wakati ambapo mawasiliano ya kielektroniki
yanaweza kupokelewa na mlengwa katika anwani
hiyo; na
(b) mlengwa
anajua
kuwa
mawasiliano
ya
kielektroniki yametumwa kwenye anwani hiyo.
(5)
Endapo mlengwa hajatenga mfumo wa
mawasiliano, upokeaji wa taarifa unatimia pale ambapo
mawasiliano ya kielektroniki yanapokelewa na mlengwa, au
yalitakiwa katika kikawaida yakupokelewa na mlengwa.
Uthibitishaji
wa upokeaji
mawasiliano

23.-(1)
Uthibitisho wa kupokea mawasiliano ya
kielektroniki, iwapo chanzo na mlengwa hawajakubaliana
kuhusu namna au njia ya mawasiliano, unaweza kutolewa
kwa(a) njia ya kielektroniki na mlengwa, ama kwa njia ya
ujumbe kujiendesha wenyewe au vinginevyo; au
(b) kwa kupitia kitendo chochote kilichofanywa na
mlengwa, ambacho kinatosha kuashiria kwa
chanzo cha mawasiliano kuwa mawasiliano ya
kielektroniki yamepokelewa.
(2) Endapo chanzo cha mawasiliano ameainishakuwa
mawasiliano ya kielektroniki yatawabana wahusika pale tu
anapopokea uthibitisho wa kupokea au unapokelewa, na
uthibitisho haujapokelewa, mwanzilishi atatakiwa(a) ndani ya muda uliotajwa au kukubalika au, iwapo
muda haujatajwa au kukubalika, ndani ya muda wa

47

Select target paragraph3