15
Na.13
Sheria ya Miamala ya Kielektroniki
2015
kumbukumbu za kielektroniki zinatakiwa kuchukuliwa au
kunakiliwa au kutunzwa kwa kuzingatia aina ya biashara au
mfumo unaotumika, au kutunza kumbukumbu ya
kielekektroniki na chanzo na madhumuni ya kumbukumbu ya
kielektroniki.
Chanzo cha
mawasiliano
ya
kielektroniki
19. Mawasiliano ya kielektroniki yatachukuliwa kuwa
yametoka kwenye chanzo iwapo yametumwa na(a) chanzo chenyewe;
(b) mtu ambaye ameidhinishwa kwa namna hiyo na
chanzo ili kufanya mawasiliano kwa njia ya
kielektroniki kuhusiana na ujumbe data; au
(c) mfumo
wa
kompyuta
katika
programu
unaojiendesha yenyewe uliyowekwa na au kwa
niaba ya chanzo.
Kuwasilisha
nyaraka
halisi katika
mfumo wa
kielektroniki
20.-(1) Endapo sheria inamtaka mtu kwasilisha
nyaraka au taarifa, matakwa hayo yatakuwa yametimizwa
iwapo(a) mtu huyo anawasilisha, kwa njia ya mawasiliano
ya kielektroniki katika mfumo wa kielektroniki,
fomu au nyaraka hiyo;
(b) kwa kuzingatia mazingira yote husika, wakati
mawasilano hayo ya kielektroniki yanatumwa,
mfumo wa kutoa taarifa ya kielektroniki ya
nyaraka hiyo ulitoa njia ya uhakika ya kuhakikisha
utunzaji wa uadilifu wa taarifa iliyoko kwenye
nyaraka;
(c) wakati mawasiliano ya kielektroniki yanatumwa,
ilikuwa ni sahihi kutarajia kuwa taarifa iliyoko
ndani ya nyaraka hiyo au taarifa ingeweza
kupatika na kwa urahisi ili kuiwezesha kutumika
katika rejea ya taarifa hiyo.
45