11
Na.13
Sheria ya Miamala ya Kielektroniki
2015
yametimizwa iwapo taarifa au nyaraka hiyo
imetumwa kwa njia ya kielektroniki.
(2) Maneno yaliyomo kwenye sheria, ikijumuisha
maneno “nyaraka”, “kumbukumbu”, “jalada”, “wasilisha”,
“peleka”, “fikisha”, “chapisha”, “andika kwenye” au maneno
au matamshi yenye maana kama hayo, yatatafsiriwa kwa
namna ambayo itaruhusu aina, mfumo au tendo hilo kuwiana
na mawasiliano ya kielektroniki isipokuwa kama imeelezwa
vinginevyo chini ya Sheria hii.
Mwenendo
wa mtu
anayetumia
saini ya
kielektroniki
12. Mtu anayetumia saini ya kielektroniki atawajibika
kisheria kwa kushindwa kuchukua hatua stahiki kuthibitisha(a) kuhakikisha uhalali wa saini inayotumika; na
(b) uhalali wa cheti au kuzingatia masharti yanayo
husiana na cheti iwapo saini ya kielektroniki
inawiana na cheti.
SEHEMU YA TATU
HUDUMA ZA SERIKALI MTANDAO
Utambuzi wa
huduma za
Serikali
mitandao
13.-(1) Bila ya kuathiri sheria nyingine yoyote,
ambapo taasisi ya umma ina mamlaka ya kushughulikia
taarifa au nyaraka au kutoa huduma, inaweza kushughulikia
taarifa au nyaraka hiyo au kutoa huduma hizo kwa njia ya
kielektroniki kwa mujibu wa Sheria hii.
(2) Masharti kuwa taarifa au nyaraka itatolewa
kimaandishi au kusainiwa haitatafsiriwa kuzuia matumizi ya
njia ya kielektroniki.
(3) Taasisi ya umma inaweza kuchukua au kupokea
malipo kwa njia ya kielektroniki kwa namna
itakavyoainishwa.
(4) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo cha
(1), Waziri anaweza kwa kushauriana na Waziri
mwenye dhamana na masuala ya Serikali Mtandao
na kwa Tangazo litakalo chapishwa kwenye Gazeti
la Serikali, kutoa miongozo itakayo ainisha-
41