Na.13
Sheria ya Miamala ya Kielektroniki
2015
10
Uthibitisho
10. Endapo sheria inahitaji(a) saini, maelezo au nyaraka kuthibitishwa, rasmi,
kukubaliwa, kuidhinishwa au kutolewa chini ya
kiapo, masharti hayo yatachukuliwa kuwa
yametimizwa iwapo saini ya kielektroniki ya mtu
aliyeidhinishwa
kutekeleza
wajibu
huo
imeambatanishwa, imejumuishwa au katika hali ya
kawaida inahusishwa na saini ya kielektroniki au
ujumbe wa data;
(b) mtu kutoa nakala ya nyaraka iliyoidhinishwa rasmi
na nyaraka hiyo ipo katika mfumo wa
kielektroniki,
masharti
hayo
yatakuwa
yametimizwa iwapo mtu huyo atatoa nakala ya
nyaraka iliyochapishwa na kuthibitishwa.
Masharti
mengineyo
11.-(1) Endapo Sheria inahitaji(a) kuwasilishwa kwa nakala zaidi ya moja ya nyaraka
kwenda kwa mlengwa mmoja kwa wakati mmoja,
masharti hayo yatakuwa yametimizwa kwa
uwasilishaji wa wasiliano moja la kielektroniki
ambalo lina uweza wa kutolewa nakala na
mlengwa huyo;
(b) lakiri na saini kuwekwa kwenye nyaraka na sheria
hiyo haiweki utaratibu au namna ambavyo nyaraka
hiyo inaweza kufungwa au kuwekewa lakiri kwa
njia ya kielektroniki, masharti hayo yatakuwa
yametimizwa iwapo nyaraka hiyo itafungwa na
kuwekewa lakiri na kusainiwa kwa njia ya
kielektroniki na mtu ambaye alitakiwa kusaini na
kuweka lakiri nyaraka hiyo;
(c) mtu kutuma taarifa au nyaraka kwa njia ya posta
au huduma sawa na hiyo, masharti hayo yatakuwa
40