9

Na.13

Sheria ya Miamala ya Kielektroniki

2015

Matumizi ya
saini salama
ya
kielektroniki

8. Saini salama ya kielektroniki itachukuliwa kuwa
imetumika iwapo:
(a) imetumwa na mmiliki wa saini salama ya
kielektroniki;
(b) inawekwa na mmiliki kwa lengo la kusaini au
kuthibitisha mawasiliano hayo ya kielektroniki.

Kutunza
kumbukumbu
kielektroniki

9.-(1) Endapo sheria inahitaji taarifa fulani au nyaraka
kutunzwa, masharti hayo yatakuwa yametimizwa kwa
kutumia taarifa ya kielektroniki, ilimradi masharti yafuatayo
yatazingatiwa:
(a) taarifa iliyomo kwenye kumbukumbu hiyo ipo
katika njia ya kielektroniki,
(b) kumbukumbu ya kielektroniki inashikiliwa au
kuwekwa katika namna ambayo imezalishwa,
imetumwa au imepokelewa au ipo katika
mpangilio ambao umewekwa wazi ili kuonyesha
taarifa hiyo ni saini; na
(c) taarifa hiyo ya kielektroniki inashikiliwa au
inatunzwa katika namna ambayo inawezesha
utambuzi wa chanzo na sehemu ambayo taarifa
hiyo ya kielektroniki au mawasiliano ya
kielektroniki yanaelekea na tarehe na muda ambao
ilitengenezwa au ilizalishwa, ilitumwa, ilipokelewa
au kutunzwa.
(2)
Wajibu wa kushikilia au kutunza nyaraka,
kumbukumbu au taarifa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha
(1) hautahusu taarifa yoyote ambayo madhumuni yake
pekeeni ni kuwezesha ujumbe kutumwa au kupokelewa.

39

Select target paragraph3