Na.13

Sheria ya Miamala ya Kielektroniki

2015

8

(c) ina uwezo wa kuhifadhiwa na mtu huyo mwingine.
(2)
Kifungu kidogo cha (2) kitatumika iwapo
maelekezo ya kuwa katika maandishi ni ya lazima au iwapo
sheria inaainisha madhara ya taarifa ambayo haiko
kimaandishi.
Saini ya
kielektroniki

Saini salama
ya
kielektroniki

6.-(1) Endapo sheria inahitaji saini ya mtu, kuwekwa
masharti hayo yatatimizwa kwa kuweka salama na saini ya
kielektroniki iliyowekwa chini ya Sheria hii.
(2) Masharti yanayohitaji saini ya kielektroniki chini
ya kifungu kidogo cha (1) yatakuwa yametimizwa iwapo:
(a) njia hiyo inatumika kumtambua huyo mtu na
kuonesha nia ya mtu huyo kuhusu taarifa
iliwasilishwa;
(b) wakati wa matumizi ya njia hiyo, njia hiyo ilikuwa
inaaminika na sahihi kwa madhumuni ambayo
taarifa ilimesilishwa.
(3) Wahusika katika mkataba wanaweza kukubaliana
kutumia njia fulani ya kusiani ya kielektroniki kwa kadri
watakavyoona inafaa, isipokuwa kama imeelezewa
vinginevyo na sheria.
7. Saini ya kielektroniki itachukuliwa kuwa ni salama
iwapo:
(a) ni ya kipekee kwa madhumuni ambayo inatumika;
(b) inaweza kutumika kumtambua mtu ambaye
anasaini mawasiliano ya kielektroniki;
(c) inatengenezwa na kuwekwa kwenye mfumo wa
mawasiliano ya kielektroniki na mweka saini;
(d) ipo chini ya udhibiti wa mweka saini; na
(e) imetengenezwa na
kuunganishwa
kwenye
mawasiliano ya kielektroniki ambayo inahusiana
nayo kwa namna ambayo iwapo kuna mabadiliko
yoyote yanafanyika kwenye mawasiliano ya
kielektroniki, mabadiliko hayo yatafichuliwa.

38

Select target paragraph3